Dec 1, 2008

Tusisherehekee ila tujutie na tujifunzetusipojitazama na kuchukulia maanani sidhani kama huyu alizaliwa hivi. shauri yako we sherehekea tu siku ya ukimwi duniani halafu ujisahau

Usiku wa Kujiachia unakaribia ndani ya dodoma


Mwezi disemba umewadia,na kila kona kuna pilikapilika za hapa na pale,kwenye kona ya starehe ndio usiseme,kila kona unaskia kuna tafrani flani imetokea.Sasa moja kwa moja pande za Dodoma,siku ya tarehe ishirini na nne mwezi huu kuna bonge ya Event inafanyika pande zile utakaojulikana kama 'Usiku wa Kujiachia na Ndovu' kwenye ukumbi wa Royal Village.
Hii imelengwa pande za Dodoma kwakuwa mji huo una wakazi wengi ambao wanapenda kujiachia,ukiangalia kuna vyuo vingi,wakazi wengi wajanja,hivyo siku hiyo hutakiwi kukosa....
Wasanii wengi kama Ngwear,Jay Moe,Dully Sykes,Makamua na mwingine ni suprize kwa wakazi wa Dodoma,Hutakiwi kukosa!!!!!!!!!!'
'Usiku wa Kujiachia' inaletwa kwenu na SOSARP ENTERTAINMENT pamoja na STRAIGHT FOREVER!ni booomb!

Hii ndio ratiba ya kilele cha burudani ndani ya clouds fm


e bwana eeeee baada ya shangwe za kutosha mwaka 2008 kutoka kwa mwanadada kat deluna sasa ni wakati wa kilele cha burudani zoooooooooote za mwaka huu.eeeee bababa

1. kwanza kabisa litapigwa bonge la beach party mchana kweupeeeeee na mabo kibao ya kimwambao,host wakati wanaowakilisha double xl hot 3@3,listening party ya album ya shangwe pamoja na perfomance kutoka kwa wasanii waliowakilisha ndani ya lbum hiyo.KIINGILIO IKIWA NI TICKET YAKO YA KUINGILIA TAREHE NANE PALE GYMKANA YAANI BUKU 10 PARTY 2.

2. kilele chenyewe sasa ambapo the first lady wa rough rider EVE atapagawisha jukwaani pamoja na the heavy weight mc akiwakilisha terror squad FAT JOE, na ticket ni buku 10 tu kama utanunua tiket yako mapema na elfu 15 kama utataka kutumwagia mafaida.ni kilele cha burudani yaani streight music climax, clouds fm pamoja na prime time promotion.

Hali si mbaya kwa chamillion wa uganda


baada ya ndoto iliyomsababishia kujirusha kutoka ghorofa ya pili mjini arusha siku moja kabla ya fiesta ya kwanza mjini tamga alipotakiwa kupafom na kumsababishia kuvunjika kwa miguu yake yote miwili, kama inavyooshesha hapo juu mchizi anaendelea fresh.tuomuobee mungu, makamuzi yanaweza rudi kama mwanzo si unajua shangwe zake stejini.