May 20, 2013

AFANDE SELE ASUSA KULA SIKU MBILI BAADA YA SIMBA KUFUNGWA

Jumamosi (May 18) kulikuwa na mpambano wa watani wajadi Simba na Yanga na timu ya Simba iliupoteza mchezo huo kwa kufungwa magoli 2 kwa bila na Yanga.
King Selemani ama Afande Sele kutoka mji kasoro bahari Morogoro ni moja ya watu wanaonekana kuwa ‘addicted’ na ushabiki wa soka kiasi cha kushindwa kuvumilia maumivu ya kufungwa kwa timu anayoishabikia, Simba kitendo kilichompelekea asuse kula toka Jumamosi.
Akizungumza na Suddy Brown katika U Heard kupitia XXL ya Clouds FM, mke wa rapper huyo mkongwe Mama Tunda, amethibitisha kuwa mumewe amegoma kula toka siku ya mechi.
pole sana Afande Sele...!!!!!

0 comments:

Post a Comment