May 21, 2013

USIKU WA HIP HOP NA FAINALI ZA VODACOM MIC KING KUFANYIKA MEI 25

   Uongozi wa kampuni ya Dar Live Co.Ltd unatarajia kufanya tamasha kubwa la kila mwaka la usiku wa Hip Hop,Jumamosi hii, Mei 25,2013 katika ukumbi wa burudani Dar Live,uliyopo Mbagala Zakhem au kwa jina lingine Mbagala Rangi Tatu.Usiku wa Hip Hop mwaka huu utafanyika pamoja na fainali za kumtafuta mkali wa Mic,fainali ambazo zimeandaliwa kwa pamoja na kampuni ya simu za mkono ya Vodacom.Fainali hizi zinajulikana kwa jina la THE VODACOM MIC KING, na mshindi ataondoka na gari la kisasa aina ya TOYOTA FUNCARGO,(New Model) lenye thamani ya shilingi milioni 15

                                                              Stamina na John Dilinga

                                                                          John Dilinga
Hawa ndiyo washiriki watakaochuana Mei 25, mshindi ataondoka na zawadi ya gari lenye thamani ya shilingi milioni 15

0 comments:

Post a Comment