Thursday, April 24, 2014

Ndugu na marafiki wa Mwanaisha washangazwa Chidi Benz kupewa dhamana licha ya aliempiga kuwa na hali mbaya


Juma nne (22 April) tuliripoti habari zilizomhusisha rapper Chidi Benz kumjeruhi vibaya aliewahi kuwa mpenzi wake "Mwanaisha Kiboye" kwa kile kilichodaiwa kumuita kwa nguvu wakati Chidi Kipita na mpenzi wake mpya. 
Mwanaisha aliharibika vibaya maeneo ya usoni na kusababisha kushonwa nyuzi 18 nauso pamoja na kichwa kuvimba na kumsababisha kuzimia kila wakati.
Rafiki wa Mwanaisha amesikitishwa kuskia kuwa Chidi ametoka kwa dahamana ya shilingi laki moja licha ya kuwa hali ya mgonjwa ni mbaya mpaka kufikia kuthibitishwa na hakim pamoja na mkuu wa kituo.

Mabest kuzindua documentary ya maisha yake jumapili hii

Msanii Mabeste anatarajia kuzindua Documentary itakayoonyesha maisha yake halisi, kuanzia wapi aliptoka,  hustle alizopitia mpaka wapi anapoelekea kwa sasa.
"Ducumentary hiyo mpaka sasa ina dakika zaidi ya 40, na nitakuwa nikiizindua kwa episod, so episod ya kwanza nitaizingua pale Billcanas jumapili hii, na nitaendela na episod zingine katika kumbi zingine." amesema Mabeste.

Video: Zijue nyimbo alizowahi kuandika Victoria Kimani, wapo Timberland na Chrisbrown


Nilipoona alichokipost dadiva kutoka Kenya "Victoria Kimani" ambae ameishi Marekani zaidi ya robo tatu ya maisha yake katika akaunti yake ya Instagram, mwenyewe nilibaki kushangaa. Kumbe licha ya kujikita kwenye muziki muda si mrefu, Kimani alikuwa ni mwandishi mzuri tu wa nyimbo.Leo hii amefunguka kwa kutaja nyimbo alizowahi kuandika.

Video queen amfungulia mashtaka 50 Cent kwa kumkashif na kumharibia kazi yake

Baada ya kutapakaa kwa picha ya matukio ya utengenezaji wa video ya wimbo wa 50 Cent, 50 alichukua uamuzi wa kuandika katika akaunti yake ya instagram yenye wafuasi zaidi ya milioni 8 na kumkashifu video queen aliekuwa akifanya nae kazi katika video hiyo kwa kumtuhumu kuwa yeye ndio amesambaza picha hizo.
kupitia Instagram na twitter 50 aliandika aliwaonya watu wasifanye kazi na mwanadada huyo na kumuita malaya mwenye kiu na video,
 "WARNING: Do not attempt to work with this thirsty video bitch."

Audio na Video: Baada ya muda mrefu BOB na Micharazo wamedondosha audio na video "Mambo Mengine Baadae"

BOB na Micharazo leo hii wamedondosha bonge la pini "Mambo Mengine Baadae" akiwemo Nyadu Toz, Mr Blue na Uswege. fanya kuitizama hapao chini 

People Magazine wamtangaza Lupita Nyong'o the most Beautiful Star 2014

Mwaka jana  ulikuwa ni mwaka mzuri sana kwa Lupita baada ya kupata nafasi ya kuigiza kwenye movie "12 Years A Slave". lakini mwaka 2014 unaokana kuchanua zaidi kwake kuzidi mwaka uliopita sio tu kwa kushinda tuzo ya Oscar kama "Best Supporting Actress " lakini pia Nyong'o (31) amepewa tittle na  People magazine ya kuwa the most Beautiful woman.
akiongea na magazine hiyo Lupita amesema, alipokuwa mdogo alidhani tafsiri ya mwanamke mrembo ni yule mwenye ngozi nyeupe na nywele ndefu zinazining'inia.

Wednesday, April 23, 2014

Beyonce na Jay Z hawatahudhuria harusi ya Kanye na Kim

Mwezi uliopita (March) kulikuwa na tetetsi kuwa Jay Z ametupilia mpali ombi la Kanye West kumtaka kuwa best man kwenye harusi yake, sasa kuna habari zinazosema kuwa Jay Zhana hat ampango wa kutokea kabisa kwenye harusi yao.
Chanzo kinadai kuw Jay angeweza kutokea kama isingekuwa ni public event, na kuwepo kwa camera nyingi za E pamoja na kutokea kwenye reality show (keeping up with the kardashians).

Matumizi mabaya ya dawa ya kifua kwa asanii yasababisha kutokutengenezwa tena kwa dawa hizo


Kampuni ya kutengeneza dawa za kikohozi"Actavis" yasitisha uzalishaji na mauzo ya dawa za  "Promethazine Codeine" na kuziondoa katika sok, kutokana na matumizi mabaya ya dawa hizo kwa wasanii wengi wakubwa wa Marekani.

Msemaji wa kampuni hiyo amesema kutokana na attention kubwa iliyotolewa na vyombo vua habari Actavis imetoa uamuzi wa kusitisha uzalisha na mauzo ya dawa hizo.msemaji huyo ameongeza kwa kusema kuwa attention hiyo imeipamba matumizi ya dawa hizo ambayo ni kinyume na sheria na hatari ambayo ni tofauti na matumzi halali ya dawa hizo.

Picha: Wasanii waungana kutengeneza wimbo na video ya wimbo wa muungano

Wasanii zaidi ya 50 wa Bongo Flava, Hip Hop, Injili, Dance na Taarab wameungana pamoja na kufanya wimbo wa kuhamasisha Muungano unaotoka April 26, 2014.

Wasanii wa Tanzania kuanzia muziki, kwaya,dance mpaka bongo movie, wameungana kwa pamoja na kutengeneza wimbo wa pamoja kuhusu Muungano ambao kilele kitakakuwa siku ya ya tarehe 26 mwezi huu.
Wimbo huo umejumiaisha wasanii kama Mabeste, Diamond, Ommy Dimpoz, Lina, Khadija Kopa, Manddojo na Domo Kaya, Mwana FA, AT,AY,Mrisho Mpoto,Madee,Asley,Chege, Qeen Darlin, Mwasitina wengine kibaona kutengenezwa na Tuddy Thomas na kusimamiwa upande wa video na Raqie kutoka I-View Media

DESIGNED

THIS BLOG IS DESIGNED BY DESY ERNEST | PHONE NUMBER : +255-714-890-227 | EMAIL : desy@g5click.com