May 1, 2012

J.LO, IGLESIA NA Y YANDEL WATANGAZA TOUR YAO YA PAMOJA KIPINDI CHA JOTO.

Jennifer Lopez, Enrique Iglesia na Y Yandel wametangaza Tour yao ya pamoja katika kipindi cha joto kinachokuja (Summertime). Jumatatu iliyopita huko Los Angeles kwamba the 20 city MEGA concert itaanza July 14 huko Montreal.
"Tutawapatia kila kitu tulichanacho kwa ajili yao, nadhani itakuwa moja kati ya Tour za kihistoria, kwa sababu sijui kama imeshawahi kutokea ambapo walatino tumekutana kama family" Alisema J.Lo.

Iglesias alisema Tour itahusisha hit songz zao wataperform pamoja. " Na ngoma kibao na Wisin Y Yandel na Jennifer pia" Aliuambia umati wa watu.
J.lo atakuwepo na watoto wake mapacha Max na Emme watakuwepo kwenye Tour bus hilo.

MAKING VIDEO YA WHERE HAVE YOU BEEN PART 3 BY RIRI.(RIHANNA).

RICH MOKO AKIINGIA SELO MSIMBAZI.

Rich one akiingia kituo cha polisi Msimbazi, check body language ya askari anaandikisha anacheka Rich one mwenyewe hana wasiwasi hata kidogo, inasemekana eti anatumia jina la Ally Kiba kujipatia fedha isivyo halali, kuomba pesa na kutapeli watu kwamba yeye ni Ally Kiba kwa njia ya simu,wametrack mtandao ndo akakamatwa yeye, Bado tunasikilizia itakavyokuwa alafu more stories hapa http://www.djfetty.blogspot.com/ we have nothing much to say tukawa tunahukumu kumbe wanajuana tusubiri shauri hili mwisho wake huko mahamakani na polisi alafu tutajua mpango mzima, kwani hatuna tatizo na mtu pia tutamtamfuta Rich Moko abonge piaaaaaaaaa! Lakini daaaaah nouuuuuuumer.

JAY – Z ADIZAINI LOGO MPYA YA TEAM BROOKLYN NETS.
Hov, Jiga Man, Blue Ivy’s dad, The man himself JAY Z amedizaini logo mpya kwa ajili ya Brooklyn team, logo hiyo inamuonekano wa rangi nyeusi na nyeupe, wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa wa Basketball Brett Yorkmark alinukuliwa akisema “ Leo tunazindua chapta nyingine, Hii iko fresh sana, tumesubiri miaka saba (7) mpaka kufikia hapa”.

Muonekano wa kibiashara wa team tayari unaonekana kupitia NJNets.com , wakati huo huo vitu vingine vya ziada unaweza kuviona kwenye face book page ya team zikiwemo kofia, tops na tishets.

LIL WAYNE AMALIZA KESI YA MADAI NJE YA MAHAKAMA.

Mkali kutoka New Orleans, mirror featuring Bruno Mars singer Lil Wayne a.k.a Wizia babes amemaliza kesi nje ya mahakama, Kwa mujibu wa TMZ kesi hiyo ilikuwa ni ya madai iliyofunguliwa March mwaka 2011 ikimshtaki Wayne kwa kutomalizia malipo ya ngoma ngoma lolpop na other tracks zilizokuwemo katika album ya mwaka 2008 “Tha carter III” kiasi alichokua akidai ni dola milioni 20 . Producer huyo anayeitwa “Deezle” Harrison amelipwa pesa hizo dola million 20 na kesi hiyo kufutwa.

Deezle hakuwa producer pekee aliyelalamika, Play N- Skills walimshtaki Weezy mwezi June 2011 kwa kutolipa malipo ya LP ya royalties, mwingine alikuwa David Kirkwood mwezi huo huo.

RIHANNA AKWAPUA CAMERA YA PAPARAZI AKIWA UFUKWENI HUKO HAWAII.

Mwanadadiva mkali wa ngoma Cheers na nyingine kali nyingi Rihanna a.k.a Riri, akiwa ufukweni huko Hawaii katika mapumziko ya weekend Riri alijikuta akifuatiliwa na waandishi wa habari akiwa amevalia kofia ya kicowboy na bitsy bikini alimsogelea mwandishi huyo na kunyakua camera yake, rafiki yake aliyekuwa pembeni akapiga picha tukio hilo, muda mfupi Riri akatweet ili rafiki zake kwenye twitter ambao ni zaidi ya watu milioni 18 waone. Tweet yake iliandika " Me high jacking a papz" sehemu hiyo ya kunyangwa camera kwa muandishi huyo ilikuwa ni sehemu ya kuhave fun lakini waandishi ilibidi watulie tu, baada ya tukio hilo Riri aliendelea kula bata na washkaji hao. Akatweet tena " Haya sindo maisha, inakuwje kama unawafanya paparazi waingie kwenye maji na wapige picha na wewe".

Jamaa wamesahau kazi wakajichanganya na Rihanna kabla wajapeleka ofisini mzigo wafanye stories wakafanyiwa wao story, mmoja ya watu waliokuwepo eneo lile (marafiki) wakapiga picha akatengeneza businness cards yenye picha yake na Rihanna. " kuna mmoja amenipa business card yenye picha yangu na yeye.....poor dat".
Matukio kama haya sio mageni kwa Rihanna mara nyingi hua anatweet kila matukio anayoyafanya kwa hiyo journalists hakuna kazi sana ya kumfuatilia coz anatoa up date za anachokifanya mara kwa mara.Ukimfuatilia karibu anakuafanyia story hii kali sana journalists jipange mzeeiyah..